Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 11, 2013

SIMBA YASEMA MAANDALIZI YA MCHEZO DHIDI YA LIBOLO YA ANGOLA YAPO VEMA

Uongozi wa klabu bingwa nchini Simba umesema kuwa unaendeleea vizuri na maandalizi ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu kutoka nchini Angola ya Libolo.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema meendeleo ya kambi na mazoezi yao mjini Arusha yanakwenda vizuri.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga imesema hali ya kikosi ni nzuri morali ya wachezaji iko juu na hakuna mgogoro au matatizo yoyote.
Paulo Ngalema.
Majeruhi mpya ni mchezaji Paulo Ngalema ambaye aliumia goti katika mechi ya juzi dhidi ya Oljoro JKT. Mchezaji huyo tayari amesafirishwa kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi zaidi.

Kutokana na tatizo hilo, Ngalema hataweza kucheza katika ijayo dhidi ya Libolo ya Angola katika Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo.

Kupitia taarifa hiyo uongozi wa Simba umewataarifu wapenzi na washabiki wake kwamba hali ya timu ni shwari kabisa. Hakuna mchezaji yeyote aliyefungiwa wala kusimamishwa na hakuna mitafuruku baina ya wachezaji na makocha au wachezaji na viongozi wa klabu.

Simba SC pia inakanusha taarifa zozote za wachezaji wake au makocha wake kupigwa (au kutaka kupigwa) mara baada ya mechi ya Arusha.
Kwa waliokuwapo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta siku ya Jumamosi mara baada ya mechi dhidi ya Oljoro, watakuwa mashahidi kwamba baadhi ya wachezaji wa Simba walibebwa na washabiki na Mrisho Ngassa alipewa zawadi ya Sh 10,000 na shabiki mmoja kutokana na mchezo wake.

Washabiki walifahamu kuwa matokeo yale ya 1-1 yalikuwa ni sehemu ya mchezo.
Taarifa za kuwapo kwa vurugu zimetiwa chumvi kwa sababu ambazo klabu yetu haizifahamu.

Simba SC inaomba washabiki wake wawe watulivu na werevu katika wakati huu ambapo tunajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Umoja wa washabiki ndiyo utakaosaidia na si mtengamano.

No comments:

Post a Comment