Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 10, 2013

SIMBA HOI KWA OLJORO JKT YATOKA SARE 1-1


Wachezaji wa simba, wakimpongeza kiungo wao Mwinyi Kazimoto, baada ya kuifungia timu yake bao, wakati wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha jana.
*************************************
TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, jana ilivutwa shati na JKT Oljoro baada ya kufungana bao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwa timu ya Simba  imetimiza sare ya pili tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare kama hiyo na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuifanya 
Simba kutimiza jumla ya  pointi 28, baada ya kucheza mechi 16, huku watani wao Yanga wakiongoza kwa kuwa na pointi 33 na mchezo mmoja mkononi, wakati Azam FC ya pili wakiwa na pointi 30 na mchezo mmoja mkononi.
Bao la JKT Oljoro, lilifungwa na Paul Nonga, katika dakika ya tisa tu tangu kuanza kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment