Mchezaji
wa timu ya waendesha Bodaboda kutoka Tegeta akiwania mpira mbele ya
mchezaji wa timu ya Waendesha Bodaboda kutoka Kawe katika mashindano ya
ligi ya Bodaboda inayoendeshwa na Jeshi la polisi kikosi cha usalama
barabarani ambapo timu ya Kawe imeifunga timu ya Tegeta kwa magoli 3-0
kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe jijini
Dar es salaam.
Mashindano
hayo yanashirikisha timu za mkoa kipolisi wa Kinondoni ambazo zinatoka
katika maeneo ya Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo wachezaji
wakiwa ni waendesha Booda, awamu ya kwanza ya ligi hiyo ilikuwa na timu
32 na sasa ni awamu ya pili ambapo timu 16 zinashindana ili kupata timu 8
zitakazoshiriki Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata mshindi wa
mashindano hayo ya Kinondoni Bodaboda ambaye atapata zawadi nono.
Lengo
la Mashindano hayo ni kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa
kipolisi wa Kinondoni ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia ili
jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha juu
ya sheria za usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye
uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
Mkaguzi
msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Agatha Isack
akimtakia uchezeshaji mwema mshika kibendera wa kushoto Hamis Pondamali
kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers
jijini Dar es salaam.
Timu ya Kawe ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo na kupata mawaidha mawili matatu.
Kikosi
cha timu ya Tegeta kikiwa katika picha ya pamoja kalba ya kuanza kwa
mchezo huo timu hiyo imefungwa magoli 3-0 na timu ya Kawe.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
Wachezaji
wa timu za Kawe na Tegeta wakiwania mpira uliojuu wakati wa
mchezouliokutanisha timu hizo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe
jijini Dar es salaam
Kutoka
kulia ni Agatha Isack Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani, Esther Ngaja Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani, mwamuzi wa mchezo huo Geofrey Mwamboneke, mwamuzi msaidizi namba moja Hamis Pondamali, na mwamuzi msaidizi namba 2 Mwanahamisi Matiku,
ASP. Emilian Kamuhanda Insp.Soud Ramadhan na Mratibu wa kombe hilo
Ernest Mbaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa
mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers.
No comments:
Post a Comment