Leordigar Chilla Tenga amesema kuwa alishauriwa
visivyo juu ya kuwepo fursa ya maombi ya mapitio ya maamuzi ya kamati ya Rufaa
ya uchaguzi kwa wagombea walioenguliwa na kamati
hiyo.
Tenga ametoa
kauli hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo ambapo
amesema chama cha mpira kiliunda vyombo vyake vya kimaamuzi kwa taratibu na
kwamba maamuzi ya vyombo hivyo yanapaswa
kuheshimiwa.
Amesema ni
kweli alitamka kuwa wagomboea walioenguliwa katika kinyanganyoro hicho cha
uchaguzi kufuata taratibu ambapo alieleza waandishi wa habari juu ya fursa tatu
za mwisho kupitia baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya Iddi
Mtinginjola kumalizika.
Amesema
hatua ya kwanza aliyopendekeza ilikuwa review, kwenda fifa na ikishindikina basi
ni kwenda CAS.
Amesema kuwa
TFF haina tatizo na maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi kwa kuwa jambo hilo
limepitia katika mikono ya sheria na kwamba inawezekana kukajitokeza mitazamo
tofauti ya tafsiri ya kisheria, hivyo wanaheshimi maamuzi ya chombo hicho
ambacho kimeundwa kwa kufuata utaratibu.
Rais Tenga
amesema kwa vile hicho ndicho chombo cha mwisho nchini katika masuala ya
uchaguzi alishauriwa kuwa kingeweza kufanya review.
“Kwa vile
hakuna chombo kingine, nikashauriwa kuwa kinaweza kufanya review. Katika
utaratibu wa kutoa haki, uamuzi ni lazima uwe wa wazi kwa kutoa sababu.
Nilidhani hilo linawezekana, kwani Mahakama Kuu hufanya hivyo. Kwa hili uamuzi
wa Mtiginjola ni sahihi,” amesema Rais Tenga.
Kamati ya
Mtiginjola iliyokutana jana (Februari 18 mwaka huu) ilitupa maombi ya review
yaliyowasilishwa mbele yake na waombaji uongozi watano kwa vile hakuna kipengele
chochote kwenye Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi kinachotoa fursa
hiyo.
Waombaji
hao walikuwa Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad
Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi
Kuu (TPL Board).
Wengine ni
walioomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye
mabano; Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na
Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na
Simiyu).
No comments:
Post a Comment