RAIS wa Nigeria, Goodluck Jonathan
amekipongeza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Super Eagles kwa
kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika-Afcon baada ya kuifunga Burkina Faso kwa
bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa jana katika Uwanja wa Taifa jijini
Johannesburg, Afrika Kusini
Katika taarifa iliyotolewa ofisini
kwake rais Jonathan alimshukuru kocha Stephen Keshi, wachezaji na viongozi wote
ambao walifanya kazi ngumu kuifanya Super Eagles kupata ubingwa wa kujivunia
baada ya miaka 19 kupita. Rais pia anaamini kwa ushindi huo
waliopata katika Afcon itakuwa chachu ya mafanikio zaidi huko mbele hususani
katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil
mwakani.
Jonathan
aliishukuru serikali ya Afrika Kusini na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF
kwa maandalizi mazuri ya michuano hiyo na kuahidi kuwaandalia mapokezi makubwa
Super Eagles pindi watakapotua jijini Abuja, Jumanne. Bao pekee lililoipa ushindi Super
Eagles na kukata kiu yao ya miaka 19 ya kulikosa kombe hilo lilifungwa na
mchezaji ambaye anacheza katika timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Nigeria Sunday
Mba.
Matokeo hayo pia
yanamuingiza Keshi katika vitabu vya kumbukumbu akiwa kocha wa pili kushinda
kombe hilo akiwa kama mchezaji na baadae kocha, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa
marehemu Mahmoud El Gohary wa Misri.
Shangwe na furaha:
wachezaji wa Nigeria wakinyanyua juu kombe la ubingwa ikiwa ni mara ya tatu
kulinyakua katika historia ya fainali hizo.
|
Nigeria imefanikiwa kuchukua kwa mara ya tatu taji la soka la mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Bukina Faso
bao 1-0 huku Nigeria ikitawala
mchezo wa fainali uliopigwa
jijini Johannesburg.
Sunday Mba aliifungia Nigeria maarufu kama 'Super Eagles' bao hilo zuri kwa mpira wa
kubetua na kuusukumiza wavuni mpira wa
kunyunyiza 'volley' zikiwa zimesalia dakika tano
kabla ya mapumziko baada ya muda mrefu wa kutafutana kwa tahadhari kubwa, huku pongezi kubwa zikimuangukia kocha mzalendo
na nahodha wa zamani wa timu hiyo Stephen Keshi.
Sunday Mba akijaribu
kuubetua mpira juu ya mlinzi wa Bukina Faso kabla ya kuusukumiza wavuni na kuwa
goli pekee lililo ipa ushindi Nigeria. Picha ya chini Mba na wachezaji wengine
wa Nigeria wakishangilia baada ya goli
kuingia.
Hiyo ilikuwa ni
fainali ya kwanza kwa Nigeria tangu mwaka 2000 lakini pia walikuwa
wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo tangu mapema kufuatia rikodi yao ya
kucheza michezo 12 bila ya
kufungwa.
Vincent Enyeama akipaa
angani kuunyakuwa mpira licha ya kukabiliwa na Prejuce
Nakoulma.
Baada ya Nigeria kufanikiwa kutwaa taji hilo,
mantiki yake ni kuwa kocha Keshi anakuwa
kocha wa pili kushinda taji hilo akiwa mchezaji na pia kama kocha akifuata nyayo
za Mahmoud Al Gohari wa
Misri.
Mlinda mlango wa Nigeria
Vinvent Enyeama akikabiliana na Mady
Panandetiguiri.
Victor Moses wa Nigeria
akijaribu kuuwahi mpira huku akipata upinzani kutoka kwa Bakary Kone wa Bukina
Faso(katikati), Mohamed Koffi (nyuma) na Djakaridja Kone
(kulia).
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Burkina Faso
kufikia fainali ya
michuano hiyo ambapo mwaka 1998 walifanikiwa kutinga hatua ya nufu fainali
ambapo walipoteza mchezo huo kwa waliokuwa
mabingwa Misri.
Pamoja na kufungwa
lakini walionyesha uwezo ambapo katika sehemu ya kiungo Jonathan Pitroipa
alionyesha ubunifu mkubwa na kutawala sehemu
hiyo.
Itakumbukwa Pitroipa ndiye aliyepewa kadi nyekundu kimakosa katika
mchezo wa nusu fainali dhidi ya
Ghana.
Mlinda mlango wa Burkina
Faso Daouda Diakite akizuia hatari kutoka kwa washambuliaji wa
Nigeria.
Rais wa FIFA Sepp
Blatter alikuwepo uwanjani.
No comments:
Post a Comment