Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 16, 2013

AZAM FC YAIKUNG'UTA AL NASRI YA JUBA MABAO 3-1. YAJIWEKA VIZURI DHIDI YA AL NASIR YA JUBA SUDAN KUSINI 3-1.

Mchezaji wa Azam Bolou Kipre akijaribu kumtoka mchezaji  wa Al-Nasir ya Sudan Kon James kwenye mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo huo Azam ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 huku mabao ya Azam yakifungwa na Abdi Kassim Babi na Kipre Tcheche. Picha zote na Rahel Pallangyo.
Mshambuliaji wa Azam Brian Umomy akimkimbia beki wa Al-Nasir ya Sudan Jacob Osuru kwenye mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana jioni.
Mchezaji wa Azam Kipre Tchetche akikwatuliwa na mchezaji wa beki wa Al-Nasir Joseph Odongi kwenye mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Abdi Kassim Babi akisujudu baada ya kuandika bao la kwanza la Azam katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Nasri ya Sudani Kusini.
Abdi kasim akituliza mpira.
Abdi kassima akipongezwa na wachezaji wenzake wa Azam baada ya kufunga goli la kwanza la Azam dhidi ya Al Nasri ya Juba Sudan Kusini.
Umony wa Azam akimpongeza Babi kwa kumshika kichwa baada ya kufunga goli.

No comments:

Post a Comment