Vibonde wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars
(Zambia) ambao ni Mabingwa wa Soka bara la Afrika leo
wamelazimishwa sare na Wababe wa Stars Ethiopia kwa kufungana 1-1 katika mchezo
wao wa kwanza wa kuwania ubingwa wa Afrika
Katika mchezo huo ambao Ethiopia walicheza wakiwa 10
uwanjani, walifanikiwa kufunga bao la kusawazisha katika kipindi cha
pili.
Ethiopia ambayo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya
pili baada ya kipindi cha miaka 30 kupita ilikuwa waandike goli katika dakika 20
za awali baada ya Saladin Seid kupiga mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda
mlango Kennedy Mweene.
Alikuwa ni Collins Mbesuma aliyewanyanyua mashabiki
wa Zambia uwanjani hapo na popote pale duniani baada ya kuifungia timu yake goli
katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na baadae Adane Girma aliisawazishia
Ethiopia katika kipindi cha pili.
Taifa Stars ilichezo michezo miwili ya kirafiki
dhidi ya Zambia hapa nyumbani na kushinda 1-0 na baade kucheza na Ethiopia mjini
Adis Ababa na kuchapwa goli 2-1.
Michuano ya Mwaka huu ya AFCON
imetawaliwa na sare ya bila kufungana au ya kufungana 2-2 au 1-1 huku Mali
pekee wakiibuka na ushindi hafifu wa goli 1-0
dhidi ya Niger
jana.
No comments:
Post a Comment