Friday, January 25, 2013
TAIFA STARS KUKIPIGA NA CAMEROUN FEBRUARI 6, TAYARI KIKOSI CHA CAMEROUN KIPO HADHARANI
Tanzania itacheza mchezo wa kirafiki Februari 6 mwaka huu lakini sehemu na uwanja utakaochezwa mchezwa huo bado kuwekwa hadharani.
Ingawa Cameroun wameshatangaza kikosi kitakacho shuka dimbani kuivaa Taifa stars lakini kocha wa Taifa stars bado hajafanya maandalizi yoyote ya mchezo huo.
Akizungumzia mchezo huo Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira nchini Angetile Osia amesema ni kweli wamepata mwaliko wa mchezo huo bila kufafanua zaidi.
Tanzania inakabiliwa na mchezo na Morocco wa kutafuta kufuzu fainali ya kombe la dunia 2014 Machi mwaka huu jijini Dar es salaam hivyo mchezo huu utaipa Taifa stars mazoezi zaidi
Magolikipa ni Itandje Charles (Atromitos, Greece), Mayébi Joslain (Wrexham, Wales)
Mabeki ni Nyom Allan Roméo (Grenade, Spain ), Angbwa Ossoemeyang Benoît (FC Rostov, Russia), Assou Ekotto Benoît (Tottenham, Englan), Bédimo Henri (Montpellier, France), Nkoulou Ndoubena Nicolas (Marseille, France), Kana-Biyik Jean Armel (Rennes, France), Wome Nlend Pierre (Canon, Cameroon),
Viungo wa kati ni Aminou Bouba (Coton Sport, Cameroon), Matip Joël (Schalke 04, Germany), Song Alexandre (FC Barcelone, Spain), Nguémo Landry (Bordeaux, France), Tchami Hervé (Honved Fc, Hongary), Makoun Jean II (Rennes, France), Eloundou Charles (Coton Sport, Cameroon)
Washambuliaji ni Olinga Essono Fabrice (Malaga, Spain), Emana Achille (Al-Wasl, United Arab Emirates), Eto’o Fils Samuel (Anzhi Makachkala, Russia), Aboubakar Vincent (Valenciennes, France), Yontcha Jean Paul (Sc Olhanense, Portugal)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment