Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika
ya Kusini.
RAIS wa IBF katika Bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati, Onesmo Ngowi, atasimamia pambano la ubingwa wa Dunia la
vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Februari 15, kati ya
Mkongo, Illunga Mukaba atakayekipiga na Gogita Gorgiladze wa nchini
Georgia.
Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari,
Mabondia hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12)
watapambana kugombea mkanda wa vijana wa Dunia (Youth Title) wa Shirikisho la
Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight February 15, mwaka huu.
Mpambano wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya
nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg,
nchini South Africa.
Ngowi kama Kamishna Mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na
maofisa wafuatao: Refarii: Wally
Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba
moja: Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar
(Spain) na Jaji namba tatu: Jaap
Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).
Mpambano huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF
yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa Utali wa Michezo
No comments:
Post a Comment