Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 26, 2013

IVORY COAST YA AKINA DROGBA YAIUA TUNISIA 3-0, YAWA TIMU YA KWANZA KUFUZU HATUA YA MTOANO AFCON

IVORY Coast imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuisambaratisha Tunisia kwa magoli 3-0 katika mechi yao ya Kundi D iliyomalizika punde nchini Afrika Kusini.

Winga wa Arsenal, Gervinho aliipatia Ivory Coast goli la kuongoza kwa shuti lililotinga kwenye dari baada ya kugongeana na straika wa Anzhi Mckhachkala, Lacina Traore, ambaye alimrejeshea mpira kwa pasi ya kisigino katika dakika ya 21.
Winga wa Arsenal, Gervinho aliipatia Ivory Coast goli la kuongoza kwa shuti lililotinga kwenye dari baada ya kugongeana na straika wa Anzhi Mckhachkala, Lacina Traore, ambaye
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure, alithibitisha sifa yake barani hapa baada ya kufunga goli kali la pili kwa shuti la kutokea nje ya boksi lililoenda kutinga kwenye nyavu ndogo katika dakika ya 85, kabla ya Didier Yakonan kuhitimisha ushindi mnono wa kujiamini katika dakika ya 88.

Ushindi unamaanisha kwamba Ivory Coast imetinga katika hatua ya mtoano baada ya kufikisha pointi sita. Ivory Coast imefunga magoli matano na kufungwa goli moja.
Katika mechi ya pili ya kundi hilo, Togo iliimarisha nafasi yao ya kusonga mbele baada ya kuifunga Algeria kwa magoli 2-0 na kuwa na pointi tatu sawa na Tunisia.

Straika wa Tottenham ya England, Emmanuel Adebayor aliifungia Togo goli la kuongoza kabla ya mtokea benchi Dome Wome kuipatia timu hiyo goli la pili katika dakika ya pili ya majeruhi.

Katika dakika ya 86, mechi hiyo ilisimama kwa takribani dakika 10 baada ya nguzo ya lango kulegea na kulalia upande mmoja wakati kiungo wa Algeria, Adlene Guedioura, alipotumia nyavu za lango hilo kama breki yake pale alipoingia kwa kasi wavuni katia harakati za kujaribu kufunga golini mwa Togo.


Lango hilo zima lililazimika kung'olewa na kukarabatiwa kabla ya kurejeshwa na mechi ikaendelea kuchezwa kwa takriban dakika nne kabla ya mwamuzi wa akiba kufanya jambo ambalo halikutarajiwa pale alipoinua ubao wa dakika za majeruhi na kuonyesha kuwa zimeongezwa dakika 13.

Muda huo mwingi mno ulizua maswali kwa kuwa hapakuwa na upotezaji wa muda mwingi katika kipindi cha pili. Matokeo hayo yanamaanisha kwamba Algeria wamekuwa ndiyo timu ya kwanza kuaga mashindano hayo.

Cape Verde itacheza dhidi ya Angola kesho Jumapili wakati wenyeji Afrika Kusini watawakaribisha Morocco katika mechi ambazo zitaanza kwa wakati mmoja saa 2:00 usiku.


Afrika Kusini inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne ikifuatwa na Cape Verde na Morocco zenye pointi mbili kila mmoja huku Angola ikiwa mkiani na pointi moja.

Drogba

Mchezaji wa Ivory Coast Lacina Traore akiumia baada ya kukosa goli

Yaya Toure akisukuma ngozi mbele ya Fakhreddine Ben Youssef

Hakunaga......Shabiki la Ivory Coast likiruka juu kama mmasai baada ya kuona kiwango safi leo usiku

VIKOSI:

Ivory Coast: Barry, Eboue, Bamba, Tiene, Zokora, Tiote, Toure, Romaric (Konan 88), Gervinho, Kalou (Gradel 80), Lacina Traore (Drogba 67)
Substitutes: Yeboah, Kone, Boka, Toure, Razak, Bony, Ismael Traore, Lolo, Ali Sangare
Scorers: Gervinho 21, Yaya Toure 87, Didier Ya Konan 90
Tunisia: Ben Cherifia, Ifa, Abdennour, Chammam, Ben Yahia, Traoui (Dhaouadi 86), Mouelhi, Hammami (Harbaoui 57), M'Sakni, Ben Youssef (Darragi 46), Khelifa
Substitutes: Ben Mustapha, Hichri, Baratli, Gharbi, Jemaa, Boussaidi, Khazri, Mathlouthi
Referee: Rajin Seechurn


KUNDI A
Jumapili Januari 27
[SAA 2 Usiku]
Cape Verde v Angola 17:00
Morocco v South Africa 17:00

MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi mbili]
1 South Africa Pointi 4
2 Cape Verde 2
3 Morocco 2
4 Angola 2

No comments:

Post a Comment