Burkina Faso, imeimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa robo
fainali ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika, yanayoendelea
nchini Afrika Kusini.
Kufikia sasa Tunisia inaongoza kwa magoli 3-0.
Vijana hao kutoka Magharibi mwa Afrika walipata bao lao la kwanza kunako
dakika ya 34 kupitia kwa mchezaji Alain Traore.
Baada ya kupokea pasi nzuri, Traore alivurumisha kombora kali kutoka umbali wa mita kumi, lililomuacha kipa wa Ethiopia Zerihun Tadele kimnya wazi.
Kinyume na ilivyokuwa katika mechi yao ya kwanza Ethiopia walianza kwa kufanya masihara kadhaa lakini Burkina Faso hawakuzitumia nafasi hizo kufunga.
Matumaini ya Ethiopia ya kuandikisha ushindi wao wa kwanza yalididimia pale wachezaji wake wawili walipojeruhiwa.
Ethiopia ilipata pigo pale nyota wake Adane Girma alipojeruhiwa dakika za mwanzo za mechi hiyo na mahala pake kuchukuliwa na Behailu Assefa.
Katika kipindi hicho Ethiopia vile vile ilipata pigo lingine pale kocha wake alipolazimika kufanya mabadiliko zaidi kabla ya mapunziko baada ya Asrat Megersa, kuheruhiwa na mahala pake kuchukuliwa na Yared Zinabu.
Katika kipindi cha pili, Ethiopia ilionekana kuimarika na kunako dakika ya 58 kipa wa Burkina Faso, Abdoulaye Soulama alipewa kadi nyekundu baada ya kuudaka mpira nje ya eneo lake, ili kukwepa kuchengwa na mshambuliaji wa Ethiopia.
Licha ya kipa wake wa kwanza kuondolewa, na kusalia na wachezaji kumi pekee, Burkina Faso iliendeleza mashambulio dhidi ya Ethiopia, na kunako dakika ya 72 Traore akaifungia Burkina Faso bao la pili na kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa robo fainali.
Dakika sita baadaye Burkina Faso ikafunga bao la tatu kupitia Djakaridja Kone.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa muda baada ya shabiki mmoja aliyekuwa uchi wa mnyama kuingia uwanjani na kujitumbukiza ndani ya lango la Burkina Faso.
Masaibu ya Ethiopia pale Burkina Faso walipofunga bao la nne kunako dakika ya 89.
Ushindi huo ndio kwa kwanza kwa Burkina Faso katika mashindano hayo nje ya nchi yao na ndio idadi kubwa zaidi ya magoli kuwahi kufungwa katika mechi moja tangu michuano hiyo kuanza wiki moja iliyopita nchini Afrika Kusini.
Kufatia ushindi huo, Burkina Faso sasa inaongoza kundi C ikiwa na alama nne, ikifuatwa na Zambia na Nigeria zikiwa na alama mbili kila mmoja.
Burkina nafaso sasa inahitaji kutoka sare mechi yake ya mwisho na Zambia, ili ifuzu kwa rauni ijayo.
Nahodha ya Zambia Chris Katongo amekiri kuwa ni sharti washinde mechi yao ya makundi dhidi Burkina Faso ili wafuzu kwa hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment