KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom
Tanzania, ni miongoni mwa wadhamini watakaorembesha na hatimaye
kufanikisha tamasha la tuzo za Swahili Fashion Week 2012 litakalofanyika
kuanzia kesho hadi keshokutwa.
Waandaaji wa tuzo hizo kubwa katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati tayari walishatangaza majina ya
waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili
Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zinazotumika kuwapigia kura
washiriki wa tuzo hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
alisema wapenzi wa mitindo nchini wanaweza kununua tiketi za kuingia
kwenye tamasha hilo kwa kupitia huduma yao ya M-Pesa.
Alisema tiketi hizo zinauzwa kwa Sh. 20,000 kwa ili mpenzi anaweza kununua kupitia namba +255 767 22 24 41.
Tuzo za Swahili Fashion Week 2012
zinazoenda pamoja na sherehe ya miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho
hili kubwa, mwaka huu zimeongezwa tuzo nyingine tatu kutoka katika tuzo
za mwaka jana ili kuweka changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo
nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.
Jumla ya tuzo 15 zitawaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.
Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model,
Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year,
East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality,
Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion
TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion
Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East
African Journalist (Mpya) na Upcoming Designer.
Twissa alisema: "Mchakato mzima wa
kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012
unasimamiwa na PUSH Mobile ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe
mfupi wa namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba
15678, huku mchakato mzima wa kuzihakiki kura hizo utafanywa na PKF.
Lakini pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya
www.sfw2012awards.blogspot.com."
Washindi wote wa tuzo za Swahili
Fashion Week 2012 watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili
Fashion Week, Jumamosi ya Desemba 8, 2012 katika hoteli ya Golden
Tulip, Dar es Salaam, Tanzania.
Swahili Fashion Week 2012
imedhaminiwa na: Vodacom, EATV, East Africa Radio, USAID Compete, Origin
Africa, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global
Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA
(Baraza La Sanaa Tanzania), Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania,
DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.
No comments:
Post a Comment