Draw hiyo imechezeshwa leo kwenye ofisi za TFF mbele ya waandishi wa habari na wawakilishi wa vilabu na ilisimamiwa na Salum Madadi ambaye ni Afisa maendeleo ya Soka wa shirikisho la Soka nchini.
Mashindano haya yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 11 mwaka huu, jijini Dar es salaam na yatashirikisha timu 14 ambazo zimegawanywa kwenye makundi matatu kwenye viwanja vya Azam Complex Chamazi na Karume.
Kundi A na Kundi B litakuwa na timu tano tano ambapo yatatoa timu tatu zitakazoingia robo fainali na kundi C litatoa timu 2 zitakazoingia robo fainali.
Jumla ya timu 8 zitaingia robo fainali ambayo itachezwa tarehe 18 na 19 Desemba, nusu fainali itachezwa Desemba 21 na fainali ni Desemba 23.
Kundi A lina timu za
Coastal Union
Tanzania Prison
JKT Ruvu
Mtibwa Sugar
Toto African
Kundi B
African Lyon
Polisi Moro
Azam FC
JKT Mgambo
Simba SC
KUNDI C
Kagera Sugar
JKT Oljoro
Yanga
Ruvu Shooting
RATIBA YA KUNDI A RATIBA KUNDI B RATIBA KUNDI C
Coastal Union vs Tanzania Prison African Lyon vs Polisi Moro Kagera Sugar vs JKT Oljoro
JKT Ruvu vs Mtibwa Azam vs JKT Mgambo Yanga SC vs Ruvu Shooting
Toto African vs Coastal Union Simba SC vs African Lyon JKT Oljoro vs Yanga SC
JKT Ruvu vs Tanzania Prison Azam vs Polisi Moro Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Mtibwa Sugar vs Toto African JKT Mgambo vs Simba SC Kagera Sugar vs Yanga SC
Coastal Union vs JKT Ruvu African Lyon vs Azam JKT Mgambo vs Ruvu Shooting
Tanzania Prison vs Mtibwa Polisi Moro vs JKT Mgambo
Toto African vs JKT Ruvu Simba vs Azam
Mtibwa Sugar vs Coastal Union JKT Mgambo vs African Lyon
Tanzania Prison vs Toto African Polisi Moro vs Simba
Mwandishi wa Habai akiokota karatasi zenye jina la timu na kingine chenye kundi kwenye visanduku vilivyowekwa mezani tayari kwa upangaji wa makundi |
No comments:
Post a Comment