Friday, December 14, 2012
MAANDALIZI YA PAMBANO LA CHEKA NA MMLAWI CHIMWEMWE YAKAMILIKA
MAANDALIZI la pambano la Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe toka Malawi litakalochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha yamekamilika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam promota wa pambano hilo Andrew George amesema taratibu za mchezo huo umekamilika.
"Taratibu zote za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa pamoja na kumtumia tiketi bondia Chiotka Chimwemwe", alisema George.
George alisema ameamua kulipeka pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuj kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana.
Pia alisema mabondia watapima uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.
Pambano hili litakuwa ni la raundi 12 na Mmalawi huyu anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo kuwasihi watanzania kuja kwa wingi kwani hata ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment