Timu
ya Taifa (Taifa Stars) imeingia kambini jana jioni jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa
dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) huku Kocha Kim Poulsen
akimjumuisha tena katika kikosi hicho kipa Deogratias Munishi ‘Dida’.
Kocha
Poulsen amemjumuisha tena Munishi kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya
Mwadini Ally ambaye atakuwa nje ya nchi na timu yake ya Azam inayokwenda
kushiriki mashindano maalumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC).
Wachezaji
wote wengine walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager wamesharipoti kambini hoteli ya Tansoma, na timu imeanza
mazoezi leo asubuhi (Desemba 13 mwaka huu) Uwanja wa Karume, na jioni
itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo.
Kuanzia
kesho jioni (Desemba 14 mwaka huu) itafanya mazoezi Uwanja wa Uwanja wa
Taifa wakati mazoezi ya asubuhi yataendelea kuwa Uwanja wa Karume.
Wachezaji ambao bado hawajaripoti kambini ni Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu wanaocheza mpira wa kulipwa nchini DRC.
Mechi
kati ya Taifa Stars na mabingwa hao wa Afrika itachezwa Desemba 22
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa. Kocha wa Chipolopolo, Herve Renard
ameshataja kikosi chake cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment