Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 18, 2012

CHIPUKIZI BYA ZANZIBAR YAJIPANGA NG'WE IJAYO

WAKATI ligi kuu ya soka Zanzibar ikiwa katika mapumziko hadi baada ya kumalizika sherehe za Mapinduzi mwezi ujao, timu mbalimbali za ligi hiyo zimekuwa katika harakati za kuimarisha vikosi vyao.
Katika mchakato huo, timu ya Chipukizi imeamua kuwatema wachezaji wake wanane na kuwapeleka timu mbalimbali na kusajili wachezaji watatu wapya ili kukiongezea nguvu kichosi hicho kilichopania kutwaa ubingwa wa Zanzibar msimu huu.

Naibu Katibu Mkuu wa timu hiyo Adam Abadía, amesema kuwa wachezaji hao wapya wamesajiliwa kuongeza nguvu katika nafasi ambazo zilikuwa na kasoro wakati wa hatua ya kwanza ya ligi kuu.
Hata hivyo, Katibu huyo hakuwa tayari kuyaweka hadharani majina ya wachezaji hao wapya zaidi ya kusema ni wa nafasi ya kiungo wachezaji wawili na mshambuliaji nafasi moja.
Chipukizi inatarajiwa kuweka kambi Mkoani Tanga hivi karibuni, ili kujiweka sawa kabla kwanza kwa ngwe ya pili ya ligi kuu.
Aliwataja wachezaji wanane waliotemwa na timu yake kuwa ni Vuai Abdalla aliyepelekwa Hard Rock na Ameir Daudi kwenda timu ya Machomanne, wote kwa mkopo.
Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wachezaji wa timu hiyo kuripoti mapema kujiandaa na kambi inayotarajiwa kuanza Disemba 20, mwaka huu mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment