Kocha wa serengeti boys na kocha wa Congo brazaville wakiwa kwenye press |
Timu ya taifa ya
vijana Serengeti Boys jana usiku ilifanyiwa hafla fupi ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa na kamati maalumu ya kuhamasisha watanzania kuichangia timu
hiyo pamoja kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo wake dhidi ya
timu ya vijana kutoka Congo Brazzaville ilifanyika katika hoteli ya JB Belmonte
iliyo jijini, Dar es Salaam.
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo, pamoja na
kutunisha mfuko wa Serengeti ambao inahitaji shilingi milioni 162 ili
kufanikisha azma ya kutinga fainali za mataifa ya Afrika, fainali ambazo
zitafanyika mwakani nchini Morroco.
Rais wa shirikisho
la soka nchini Leodgar Tenga alipata nafasi ya kusema machache ambapo alirejea
wito wake wa kuwataka vijana hao kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kutekeleza
maagizo ya makocha wao Jacob Michelsen na Jamhuri Kihwelu huku wakijua wazi
kuwa wamebeba roho za watanzania wengi ambao wanawaunga mkono.
Amewata kuiga mfano
wake ambapo mbali ya kuichezea timu ya Taifa katika miaka ya sabini na
themanini lakini pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ambayo ilishiriki kwa
mara ya mwisho fainali za mataifa ya Afrika.
Amewataka pia
kukumbukuka maneno mazuri aliyozungumza gwiji la zamani la soka barani Afrika
Abeid Pele ambaye alikuwepo nchini hivi karibuni ambapo mmoja wa wachezaji wa
Serengeti, Hussein Twaha alimnukuu Pele alipozungumza nao uwanja wa Karume pale
alipowatembelea maneno ambayo yaliwasisimua wadau waliokuwepo ukumbini hapo.
Alisema , “mpira
hauchezwi na watoto wa matajiri bali watoto wa maskini na kipaji pekee
hakitoshi kukupeleka kwenye mafanikio bali inahitajika juhudi binafsi” mwisho
wa kunukuu.
Kwa upande wake
makamu mwenyekiti wa kamati ya Serengeti Kassim Dewji amewataka vijana hao
kusahau maneno ya kuwa Congo imekuja na wachezaji vijeba na badala yake wafanye
kazi kuhakikisha wanawadhibiti vilivyo na ushindi upatikane.
Dewji amesema yeye
anaamini maandalizi waliyofanya vijana hao ni mazuri na kwamba wahakikishe
wanatoka na ushindi wa kishindo katika mchezo wa jumapili ili kuwapa kazi ya
ziada katika mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini Congo wiki mbili
baadaye.
Neno zuri kwa vijana
hao kutoka kwa Dewji ni kwamba anaamini watavuka hatua hiyo na wataelekea
Morroco Mwakani na kwamba baada ya fainali za Morroco basi Mungu akipenda
wachezaji zaidi ya 15 watape timu za kucheza barani Ulaya.
Naye Mwenyekiti wa
Azam mzee Said Mohamed alikumbushia namna alivyocheza soka wakati wa ujana wake
ambapo alisema alikuwa hodari katika kupenyeza mipira ya krosi ambapo alikuwa
na uwezo wa kukimbia na kupiga jambo ambalo lilikuwa likimfurahisha kocha wake na
hivyo vijana hao waige mfano wake
Juliana Matagi
Yasoda, Kaimu Mkurugenzi ya michezo Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo
amesema serikali iko nyuma ya vijana hao na kwamba imemshangaza kuona timu ya
taifa ya vijana ikifanyiwa hafla nzuri kama hiyo jambo ambalo hakuwahi kuliona
siku za nyuma.
Hata hivyo kilio
chake ni kwamba wajitume kwa kadri wawezavyo na kwamba serikali inawasapoti.
Jacob na Kihwelu
wamewahamasisha vijana kufanyia kazi yale wanayo wafundisha na kwamba wana imani
uwezo mkubwa wa kuwafunga Congo wanao.
Jamhuri Kihwelu
amesema kama wanataka kupata mafanikio na maisha mazuri katika maisha
yao, basi muda sasa umefika wa kufanya hivyo ambapo endapo watawafunga CongoBrazaville
basi kila mtu atajitokeza kuwachangia
zaidi tofauti na ilivyo sasa.
Timu hiyo ya vijana
imehashia kambi yake katika hoteli ya JB Belmonte na itaendelea kuwepo hapo
mpaka baada ya mchezo wao dhidi ya Congo Brazzaville mchezo ambao utachezwa
jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment