TIMU ya maveterani ya Simba imeshindwa kuwatambia maveterani wenzao wa Kariakoo ya Lindi baada ya kukubali kutoka sare ya 0-0 kwenye bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya TTC sigara, jijini Dar es salaam.
Bonanza hili lilihusisha timu zilizocheza ligi zamani na jumala ya timu saba zimeshiriki.
Simba ilisheheni wachezaji wake mahiri wa zamani akina Bita John, Husein Balo, Majuto Comu, Quresh Ufunguo, Damian Kimti, Barnabas Sekelo, Gabriel Emanuel, Said Msasu, Abubakar Kombo, Abdul Mashine na wengine wengi.
Mchezo huo ambao ulikuwa burudani kwa mashabiki ulishuhudia Dua Said wa Simba wakikosa penalti waliyopata dakika ya 60 baada ya mshambuliaji wao Husein Balo kufanyiwa faulo na golikipa wa Kariakoo Lindi Jumanne Ally.
Mchezo mwingine ulizikutanisha Pilsener na Reli ya Morogoro, Reli walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Salhina Mjengwa baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Mwanamtwa Kiwelu.
Bandari iliifunga Mirambo ya Tabora mabao 3-2, na magoli ya bandari
yalifungwa Kingsley Malwilo aliyefunga mabao mawili na Mohamed Hussein
na wafungaji wa Mirambo ni Paul Muhonda na Athuman Tippo
|
Kikosi cha Reli ya Morogoro na viongozi wake |
|
Kikosi cha Simba |
|
Mgeni Rasmi Jamal Rwambo akifungua bonanza |
|
Jamali Rwambo akisalimiana na wachezaji wa Mirambo ya Tabora |
|
Beki wa Kariakoo Lindi Mwamedi Pwani akimdhibiti mshambuliaji wa Simba Bita John kwenye bonanza la wachezaji wa zamani lililofanyika juzi viwanja vya TTC Sigara, mchezo ulimalizika 0-0. |
|
Kocha Mshindo Msolwa ambaye jana alikuwa anaifundisha Mirambo ya Tabora |
|
Kenedy Mwaisabula akifurahia mchezo uwanjani | |
|
Kikosi cha Kariakoo ya Lindi |
|
Kikosi cha Pilsner |
|
Kikosi cha Reli "Kiboko ya vigogog" |
|
Hapa mchezo umenoga, mgeni rasmi anatazama kwa makini |
|
Huyu ni mchezaji wa Reli alicheza dakika kumi akatoka kupumzika kwenye hema baadae akarudi, ndio mpira wa kikubwa/kiutuzima huo |
|
Mirambo Tabora hiyo wanasakata kabumbu na Bandari ya Mtwara |
|
Mbwiga ndani ya jezi kuivaa Ushirika ya Kilimanjaro lakini alitoka mapema. Sikiliza maneno yake baada ya kutoka "Mkifungwa ni nyie maana mimi ninetoka timu ipo salama" lakini walitoka suluhu |
|
Mirambo na Bandari (blue) |
|
Bwiga akiwapa mashabiki udambwiudambwi |
|
Mwamuzi wa zamani mzee Makwega |
.
No comments:
Post a Comment