MWAMUZI wa Kimataifa wa Tanzania Israel Mujuni Nkongo ameteuliwa kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha mashindano ya CECAFA maarufu kama Tusker Challenge yatakayofanyika nchini Uganda kuanzia Novemba 26 hadi Desemba 6 mwaka huu.
Nkongo ambaye ataambatana na waamuzi wasaidizi wawili wa kimataifa,Jese Erasmo toka Morogoro na Kinduli Ali toka Zanzibar.
Waamuzi wa kati wengine watakaochezesha mashindano hayo ni Thierry Nkurunzinza toka Burundi, Maeruf Mensur toka Eritrea.
Wengine ni Antony Ogwayo toka Kenya, Hakizimana Louis toka Rwanda, Ali Kalyango toka Uganda, Mohamed Hussein El Fadhil toka Sudan na Denis Bate wa Uganda
Waamuzi wasaidizi ni Mark Ssonko wa Uganda, Mussie Kinde wa Ethiopia, Peter Sabatia wa Kenya, Idam Mohammed wa Sudan, Hakizimana Ambroise wa Rwanda na Omar Abukar wa Somalia.
Makundi ya timu zitakazoshiriki mashindano haya yameshapangwa ambapo Tanzania ipo kundi B na nchi za Sudan Kaskazini, Burundi na Somalia.
Kundi A lina nchi za Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudani Kusini na Kundi C lina nchi za Rwanda, Zanzibar, Eritrea na Malawi
No comments:
Post a Comment