Mpiana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu shoo yake itakayofanyika Leaders Club Novemba 30, mwaka huu |
Mtangaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Said Kilumbanga (kulia) akiwa amepozi na wanenguaji wa mwanamuziki kutoka Congo, JB Mpiana |
MSANII nguli wa muziki wa dansi Afrika, JB
Mpiana amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kushuhudia shoo yake
itakayopigwa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Ijumaa hii,
ambapo kiingilio kwa VIP A itakuwa sh 100,000 na kawaida sh 25,000.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, JB Mpiana
alisema, anajikubali na kuithamini kazi yake ambayo anaifanya na kuahidi kuwapa
raha wapenzi na wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini ambao watajitokeza siku
hiyo.
“Kwanza nimefurahia sana mapokezi ya jana, hivyo
basi nitawapa raha siku hiyo na pia nawapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu na
kuniteua mimi kufanya nao kazi siku hiyo, nimekuja na kikosi changu kamili cha
watu 25, hivyo basi nina imani siku hiyo itakuwa raha sana,” alisema Mpiana.
Mpiana aliwataka wanamuziki wa hapa nchini,
kujituma na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuziheshimu pia, ili waweze
kufikia mafanikio ambayo wamejipangia kuyafikia, kwa kuwa hata yeye alianzia
huko na ndio sababu amefikia hapa alipo.
Naye Mkurugenzi wa QS J Mhonda Entertainment,
Joseph Mhonda, alisema kila kitu kimekamilika na kudai kuwa, kwa sasa wanasubiri
siku ifike ili watanzania wapate raha na kile ambacho wamekitarajia.
Mhonda alisema, viingilio siku hiyo itakuwa sh
25,000 kwa atakayenunua tiketi mapema, huku 30,000 kwa watakaonunulia mlangoni
na sh 100,000 VIP A kwa watakaonunua mapema huku kwa mlangoni ni sh 150,000.
No comments:
Post a Comment