HATMA ya uchaguzi wa chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa ijulikane jana sasa itajulikana Octoba 18 mwaka huu kutokana na wajumbe wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokahudhuria
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka nchini Angetile Osiah inasema kamati ilikutana Oktoba 11 mwaka huu, kujadili michakato ya chaguzi za viongozi mbalimbali na kutolea maamuzi chaguzi mbalimbali lakini la DRFA halikutolewa maamuzi
Taarifa hiyo inasema kuwa chaguzi zilizotolewa maamuzi ni ule wa chama cha sojka cha moka wa Rukwa (RUREFA), Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu (FRAT), Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) na Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es salaam (DRFA).
Pia Kamati hiyo ilijadili mchakato wa chaguzi za Chama cha Madaktari wa Michezo (TASMA) na kupokea mchakato wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mbeya (MRFA).
Kamati imeamua kuwa Uchaguzi wa FRAT ambao haukufanyika baada ya wajumbe kugoma wakipinga kuondolewa kwa baadhi ya wagombea hivyo imeagiza Kamati ya Uchaguzi ya FRAT kuhakikisha uchaguzi unafanyika Novemba 17 mwaka huu na kufanya maandalizi yote muhimu ikiwa ni pamoja na sehemu ambako uchaguzi huo utafanyika na wajumbe wa Mkutano utatakiwa kuwapigia kura wajumbe waliopitishwa kugombea uongozi tu.
Pia amesema kamati baada ya kufuta uchaguzi wa viongozi wa RUREFA na kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitaka Kamati ya Utendaji ya RUREFA kuteua kamati mpya ya uchaguzi ya chama hicho kabla ya Oktoba 20 mwaka huu na kuiagiza kamati mpya itangaze mchakato wa uchaguzi ifikapo Oktoba 24 mwaka huu.
Kamati imeamua kuwaita kwenye kikao cha kamati ya uchaguzi ya TFF kitakachokaa octoba 18 kwa maamuzi ya mwisho baadhi ya wagombea wa uongozi wa SHIREFA walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi pamoja na mwakilishi wa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA pamoja na wale walioweka pingamizi na waliokata rufaa wa chama cha soka cha soka mkoa wa Mwanza. (MRFA)
Pia kamati imeagiza TASMA ifanye uchaguzi wake Desemba mosi mwaka huu badala ya Octoba 27 mwaka huu kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchakato wa awali na kuagiza kasoro zilizojitokeza awali zinarekebishwa ili uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na Kanuni za Uchaguzi.
Angetile Osiah amesema Wagombea na wadau wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha Oktoba 18, 2012 wanataarifiwa kuwa kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF kuanzia saa 08:2012.
Kamati inawaomba wajumbe wote kuhudhuria bila ya kukosa.
No comments:
Post a Comment