Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 1, 2012

TIKETI YANGA, SIMBA KUANZA KUUZWA KESHO


Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa zitaanza kuuzwa Oktoba 2 mwaka huu kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
 
Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni.
 
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
 
Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
 

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment