SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzania limepangua tena ratiba ya ligi kuu ambapo mechi
namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu
iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani
Morogoro, sasa itafanyika Novemba 7 mwaka huu.
Mabadiliko
hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza
mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.
Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa
ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na
kituo cha televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment