Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 19, 2012

MTANZANIA MILAN MBISE AOMBEWA ICT KUCHEZA MAREKANI

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Marekani limemwombea Mchezaji Millan Mbise kutoka Tanzania Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) itakayomwezesha kucheza mpira wa miguu nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisa wa Shirikisho la Soka Nchini Boniface Wambura amesema, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Marekani (USSF) limemuombea hati hiyo Mbise kama mchezaji wa ridhaa ili ajiunge na timu ya Virginia Youth Soccer.

Pia amesema Klabu ya zamani ya mchezaji Mbise aliyezaliwa Agosti 18, 1994 imetajwa kuwa Super Sport FC, na mechi ya mwisho kwenye timu hiyo alicheza Novemba 15 mwaka juzi.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanya mawasiliano na pande husika kabla ya kutoa hati hiyo kwa mchezaji huyo kama ilivyoombwa na shirikisho hilo la Marekani.

No comments:

Post a Comment