Naye Geofrey Irick Nyange amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF, Juma Haruna Kisoma Mwakilishi wa Klabu TFF na Abubakar Allawi amechaguliwa kuwa Mhazini.
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika kisiwani Mafia ni Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus Haule na Gwamaka Oden Mlagila na mwakilishi wa Wanawake ni Florence Ambonisye.
Akiongea na waandishi wa Habari Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini(TFF) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi.
Pia aliongeza kuwa ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Pwani.
Pia alisema TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya COREFA chini ya uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Wambura alisema uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa kuzingatia katiba ya COREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
"Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF", alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment