MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa
Yanga, Didier Kavumbagu amesema wataendelea kuwapa raha mashabiki wao kwa
kushinda mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam jana kabla ya kuondoka kwenda Arusha Kavumbagu alisema ili waweze kufikia lengo la kuchukua ubingwa
wanaiona kila mechi kwa ni fainali na wanatakiwa kushinda.
Kavumbagu alisema ushindani wa
ligi hiyo, umekuwa ni mkubwa hivyo, wachezaji wenzake wanatakiwa kujituma
zaidi.
Alisema pamoja na kuanza
vibaya katika ligi hiyo, hawatakata
tamaa kutokana na wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.
Kavumbagu alisema matokeo mabaya
wanayapata hasa wanapokuwa katika mechi za ugenini na yanasababisha na waamuzi.
Alisema baadhi ya waamuzi
wanaochezesha mechi zao za ugenini hawazingatii sheria 17, kutokana na wanakuwa
na maamuzi ya upande mmoja.
“Waamuzi wanachezesha sivyo
kabisa ndio maana wanalalamikiwa sana,” alisema Kavumbagu.
Kavumbagu aliyesajiliwa na klabu
hiyo msimu huu, akitokea Atletico ya Burundi ameifungia Yanga mabao matano
tangu ilipoanza ligi hiyo, Septemba 15, mwaka huu.
Timu hiyo, ambayo juzi iliibuka
na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Morogoro, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, ilitarajia kuondoka jana kwenda
Arusha, ambako kesho itacheza na JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
No comments:
Post a Comment