Wachezaji wa akiba wa timu ya Young star wakiwa na kocha wao kwenye benchi |
Fair play!! Nahodha wa timu ya Young star akimpa huduma ya kwanza mchezaji wa Weekend |
Mchezaji wa timu ya weekend akiondosha mpira eneo la hatari |
TIMU ya Young Star ya Morogoro jana iliifunga timu ya Weekend ya Dar es salaam bao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Young Star ilijipatia mabao yake kipindi cha kwanza kupitia kwa Arshad Mianji na Osh Cozy baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wao Pedo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko, na kufanya mchezo kuonekana wa ushindani. McTIMU ya Young Star ya Morogoro juzi iliifunga timu ya Weekend ya Dar es salaam bao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Young Star ilijipatia mabao yake kipindi cha kwanza kupitia kwa Arshad Mianji na Osh Cozy baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wao Pedo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko, na kufanya mchezo kuonekana wa ushindani. Mchezaji Kamal Divecha aliifungia bao timu yake ya Weekend, bao lililodumu hadi dk 90 na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Akizungumza na DIMBA, Meneja wa timu ya Young Star Abdulmalik Hashim maarufu kama 'SUMA' alisema timu yake imecheza vizuri ndio maana wameweza kuibuka na ushindi huo.
"Ushindi tulioupata unatokana na wachezaji kuhudhuria mazoezi na kufuata mafunzo ya kocha na nimefurahi sana kwani hata wapinzani wetu ni wazuri sana", alisema Suma
Suma ambaye amewahi kuwa katibu wa Reli ya Morogoro miaka ya 80 alisema wamefurahia safari yao ya Dar na kuahidi kurudi tena kucheza michezo ya kirafiki.
Young Star yenye makazi yake mitaa ya Forest Hill inaundwa na wachezaji wenye asili ya kiasia waishio Morogoro. Mhezaji Kamal Divecha aliifungia bao timu yake ya Weekend, bao lililodumu hadi dk 90 na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO, Meneja wa timu ya Young Star Abdulmalik Hashim maarufu kama 'SUMA' alisema timu yake imecheza vizuri ndio maana wameweza kuibuka na ushindi huo.
"Ushindi tulioupata unatokana na wachezaji kuhudhuria mazoezi na kufuata mafunzo ya kocha na nimefurahi sana kwani hata wapinzani wetu ni wazuri sana", alisema Suma
Suma ambaye amewahi kuwa katibu wa Reli ya Morogoro miaka ya 80 alisema wamefurahia safari yao ya Dar na kuahidi kurudi tena kucheza michezo ya kirafiki.
Young Star yenye makazi yake mitaa ya Forest Hill inaundwa na wachezaji wenye asili ya kiasia waishio Morogoro.
No comments:
Post a Comment