MABINGWA
wa Kombe la Kagame Yanga, jana wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda
cha Kampuni ya Bia nchini (TBL), kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam,
ambacho kinaidhanmini klabu hiyo kupitia bia ya Kilmanjaro,.
Akiongea katika ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake iliamua kufanya ziara yao
katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo
yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinywaji mbali mbali, ikiwamo
Kilimanjaro.
Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager
imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo
mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri
jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi
waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa
kuthamini timu yao.
"Tunawaomba muendele na moyo huo kwani
sisi Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu
yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa
pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora," alisema Sendeu.
Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana
na kitendo cha Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda
chao, kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.
Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa
Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni
mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya
shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi, vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.
"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania
kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga imekuwa ikifanyia
mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia
timu yao.
"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe
Yanga imekuwa ya pili kuzuru TBL baada ya watani wao wa jadi kutembelea kiwanda cha Arusha walipokuwa kambini mkoani bumo.
No comments:
Post a Comment