Bwana Juma ebu walete basi vijana wako tuanze mechi si unajua mchezo ulitakiwa uanze saa 10 kamili na sasa ni saa 10;15. |
TIMU ya Yanga leo imeifunga timu ya coastal union ya Tanga bao 2-1 kwenye mchezo wa kusisimua uliochezwa Taifa .
Coastal union ambao walijipatia bao lao kupitia kwa Sud Mohamed dk 29. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Coastal wakiwa mbele kwa bao hilo moja
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kadhaa lakini Yanga ndio waliofaidika kwani kutokana na kushambulia ilifanya beki wa Coatal kujifunga wakati akiokoa cross iliopigwa na Shamte dk 85.
Dk 89 Said Bahanunzi, mshambuliaji mzawa mwenye uchu wa kufumania nyavu aliwanyanyua wanayanga baada ya kufunga bao zuri sana kwa shuti lililokwenda langoni mwa coastal union.
Tukio ambalo lilitokea uwanjani alimanusra mchezo usichezwe baada ya kocha wa Yanga Tom Saintfiet kutoa wachezaji uwanjani baada ya timu ya Coastal kucchelewa kuingia uwanjani na kung'ang\ania kuendelea kupasha bila kuja kujipanga mchezo uanze. Ni kweli ratiba inasema mchezo uanze saa 10.00 jioni lakini mchezo ulianza saa 10.30.
No comments:
Post a Comment