Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 21, 2012

TWFA YATANGAZA MAJINA YA KAMATI YA MCHAKATO WA UCHAGUZI

CHAMA cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimetangaza Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Kaimu Mwenyekiti wa TWFA, Margreth Mtaki amewaambia Waandishi wa Habari, kuwa kamati hiyo yenye wajumbe watano itaongozwa na Ombeni Zavala, na itarajia kutangaza mchakato wa uchaguzi huo Jumatatu.

Aliwataja wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jukumu la kuendesha uchaguzi wa chama hicho kuwa ni Rachel Masamu, Lloyd Nchunga, Nancy Mabula na Maneno Tamba.

Pia ametaka wadau wa mpira wa miguu wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika TWFA mara Kamati ya Uchaguzi itakapoanza mchakato.

Chama cha Mpira wa wanawake kinaingia kwenye uchanguzi mwingine baada ya kukaa kwenye madarakani kwa takribani miaka minne bila kuwa na katibu mkuu na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji baada ya uchaguzi uliopita kukosekana wagombea wenye sifa.

Kikatiba uongozi unaomaliza muda wake walitakiwa waitishe uchaguzi mdogo ndani ya siku 90 baada ya kuingia madarakani.

No comments:

Post a Comment