Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa vifaa vyenye thamani ya sh.
milioni 7.3 kwa Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambazo ni
asilimia 5 ya fedha zilizopatikana kwenye mechi ya Simba na Azam.
Mechi
hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu
mpya wa 2012/2013 ilichezwa juzi (Septemba 11 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 146, 640,000. Washabiki 26,001
walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Simba
kushinda mabao 3-2.
Sekretarieti
ya TFF inatarajia kukutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke wakati
wowote kuanzia leo ili kujua mahitaji halisi kabla ya kufanya ununuzi wa
vifaa husika.
Mgawanyo
wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 22,368,813.56, asilimia 5 ya mchango wa
kusaidia jamii (Hospitali ya Temeke) sh. 7,332,000, uwanja sh.
10,148,318.64, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
4,059,327.46, TFF sh. 10,148,318.46 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 5,074,159.32.
Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,014,831.86, kila timu sh.
32,265,025.93, asilimia 10 ya gharama za mchezo sh. 10,148,318.64, nauli
kwa waamuzi na kamishna sh. 80,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi na
kamishna 230,000, posho ya waamuzi 400,000, tiketi sh. 4,495,800,
maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na
ulinzi uwanjani sh. 2.350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh.
2,000.000.
Mchango
wa kusaidia jamii kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuzindua msimu uliopita
kati ya Yanga na Simba ulikuwa sh. 15,000,000 ambazo zilikwenda Chama
cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kusaidia uchunguzi wa kansa ya
matiti kwa akina mama.
No comments:
Post a Comment