Add caption |
MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR NAYE APATA
ITC
Shirikisho la Vyama vya Mpira wa
Miguu Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya
mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull
FC ya nchini humo.
ITC hiyo ilitumwa jana (Agosti 30
mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki
wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka
huu.
Wachezaji ambao ITC zao bado
hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya
waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani
tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba kwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa
kupatikana.
No comments:
Post a Comment