Widow’s Bay na Apple TV Zang’ara Katika Usiku wa Kwanza wa Tuzo za Ubunifu za Creative Arts Emmys 2026



Tuzo za 78 za Primetime Emmy (Creative Arts Emmys) zimetangaza washindi katika sherehe za siku mbili zilizofanyika katika Ukumbi wa Peacock huko Los Angeles, huku zikitengeneza njia kwa ajili ya usiku mkuu wa tuzo hizo utakaorushwa moja kupitia NBC na Peacock mnamo Septemba 14.

Katika sherehe hizo za wikendi hii, jumla ya tuzo 102 zilitolewa katika vipengele mbalimbali vya kiufundi na ubunifu kwa mwaka huu.

Washindi Wakubwa

Widow’s Bay (Apple TV): Imeng'ara kwa kujinyakulia tuzo 8, zikiwemo za uigizaji wa ugeni kupitia Betty Gilpin, utayarishaji wa sauti, muundo wa picha, uongozaji wa picha (cinematography), usimamizi na utunzi wa muziki, pamoja na uhariri wa sauti.

DTF: St Louis (HBO Max): Imefanya vizuri kwa upande wa vichekesho na filamu fupi, ikishinda tuzo katika vipengele vya uigizaji msaidizi (kupitia David Harbour na Linda Cardellini), huku mtengenezaji  wake Steven Conrad akizoa tuzo za uandishi na uongozaji.

Spider-Noir (Prime Video): Imeongoza katika vipengele vya uratibu wa matukio ya hatari (stunts), muundo wa vichwa vya habari, athari maalumu za kuona (VFX), na uhariri wa sauti.

The Apple Music Super Bowl LX Halftime Show Starring Bad Bunny (NBC): Imefanya vizuri sana upande wa burudani na vipindi maalum vya moja kwa moja ikiwa na tuzo 7, ikiongozwa na maonyesho na uongozaji wa kipekee wa Hamish Hamilton.

 Upande wa Majukwaa (Platforms)

Apple TV iliongoza kwa kujikusanyia tuzo 19 kwa ujumla kupitia kazi zake mbalimbali, ikifuatiwa kwa karibu na HBO Max iliyojipatia tuzo 16, wakati Netflix ikishika nafasi ya tatu kwa kujinyakulia tuzo 13.

Sherehe hizi za utangulizi zitapangiwa kurushwa rasmi katika muhtasari mmoja utakaorushwa tarehe 12 Septemba kupitia mtandao wa FXX, kabla ya kufanyika kwa kilele cha tuzo za Primetime Emmy siku ya Alhamisi, Septemba 14.

No comments