HUU NDIO UBINADAMU KUTOKA LINDI LA UMASIKINI HADI KILELE CHA DUNIA HAKIKA DOLLY PARTON NI MPIGA KINUBI WA HISIA ZA BINADAMU
Ukimtazama Dolly Parton kwenye skrini na kisha kusikiliza mashairi yake, unapata taswira kamili ya mwanamke ambaye hakuwa tu mwimbaji, bali alikuwa mpiga kinubi wa hisia za binadamu.
Unapokumbuka filamu ya The Bodyguard na jinsi wimbo wa I Will Always Love You ulivyopenya kwenye mishipa ya fahamu ya watazamaji, unagundua kuwa ulimwengu umepoteza mtu wa kipekee sana.
Kuiona ile filamu na kusikia ule wimbo uliokuwa umebeba uzito wote wa mapenzi, maumivu, na shukrani, ni kama kukumbushwa papo hapo kuwa hisia za dhati haziwezi kufichwa. Sasa mtu huyo wa hisia ameondoka, akiacha pengo ambalo halitazibwa kamwe.
Maisha ya Dolly hayakuwa ya kitoto; yalikuwa safari ndefu ya ujasiri iliyoanzia kwenye lindi la umaskini wa kutisha huko Milima ya Appalachia. Akiwa mtoto wa nne kati ya watoto kumi na wawili, alikulia katika nyumba duni ya mbao bila huduma za kisasa, akilelewa na wazazi waliomjaza upendo badala ya mali. Ukitazama maisha yake, unajiuliza kuhusu familia zetu za sasa na ustaarabu wa baadaye.
Katika maisha yake Mama yake ndiye aliyepanda mbegu ya kwanza ya muziki ndani yake kupitia nyimbo za asili na za kidini za huko vijijini. Kumbe akiwa ameiaga dunia tukitazama maiusha yake tunaona sababu ya kujiuliza na sisi.
Kupitia vibao vyake vya milele kama Jolene, wimbo uliotawaliwa na hisia za wivu na heshima kwa wakati mmoja, au Coat of Many Colors uliotokana na maisha yake ya utotoni ya kuvaliwa koti la viraka, alionesha uwezo mkubwa wa kusimulia hadithi za maisha ya kila siku.
Hata kupitia wimbo wa 9 to 5, alisimama kidete kama mtetezi wa haki za wafanyakazi wa kawaida na wanawake wa maofisini, akitumia sauti yake yenye mamlaka na mdundo wa kipekee kusukuma mabadiliko chanya kwenye jamii. Hakuwa tu malkia wa muziki wa country, bali alikuwa taasisi inayotembea iliyotumia mafanikio yake kujenga kituo cha burudani cha Dollywood na kuanzisha mfuko wa kusambaza mamilioni ya vitabu vya bure kwa watoto wadogo ili kujenga utamaduni wa kusoma duniani kote.
Urithi aliouacha unajisimamia wenyewe kama mwongozo wa jinsi ya kuishi maisha yenye maana, ukithibitisha kwamba asili ya mtu haiamui hatima yake, bali ni uthubutu, bidhi na upendo wa dhati ndio unaoweza kumbadilisha mwanadamu kutoka kwenye kibanda duni hadi kwenye kiti cha enzi cha heshima ya milele. Sasa anapoenda kupumzika baada ya kuacha mauzo ya rekodi zaidi ya milioni mia moja na utunzi wa nyimbo zaidi ya elfu tatu, dunia inabaki na alama isiyofutika ya uwepo wake.
Pumzika kwa amani, Malkia wa Country.

Post a Comment