ENG: MARYPRISCA MAHUNDI: VIJANA TUJITOKEZE KUITETEA SERIKALI DHIDI YA UCHOCHEZI MITANDAONI



Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Eng. Maryprisca Mahundi amewataka vijana kusimama kusimama imara kukemea uchochezi na upotoshwaji  unaoenezwa mitandaoni  dhidi ya Serikali.

Eng.Mahundi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa UVCCM Tawi la Chuo Cha  ADEM Kampusi ya Mbeya katika mkutano maalumu wa Tawi la UVCCM chuoni hapo.

"Tujitokeze kukemea Uchochezi dhidi ya serikali yetu unaoenezwa mitandaoni,tueleze mazuri ya serikali yetu kwa hoja" alisema Eng Mahundi.

Aidha Naibu Waziri Mahundi ambaye pia ni Mbunge Viti Maalumu anayewakilisha Wanawake UWT Mkoa wa Mbeya amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu wa nchi jambo ambalo litachangia kuwa na fursa ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato na kujiinua kiuchumi.

Amesema Vijana wanapaswa kutumia  vyema nguvu na Elimu yao  kwa kujiendeleza kiuchumi kwa kuwa Maendeleo ya nchi yanategemea zaidi Elimu na nguvu walizonazo.


No comments