Pages

Wednesday, August 30, 2023

WADAU WA MUZIKI WA DANSI WATETA NA WIZARA


 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na kikundi cha bendi ya Mlimani Park, kuhusu kushirikiana na wizara katika matukio mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao hicho kimefanyika Agosti 30, 2023 katika ofisi za wizara zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana namna bora kikundi hicho cha muziki wa densi kinaweza kutumika kuelimisha jamii kupitia muziki huo katika matamasha mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment