Pages

Wednesday, August 30, 2023

JKT QUEENS BINGWA CECAFA

 



Na Rahel Pallangyo

JKT Queens imeitwaa ubingwa michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kbaada ya kuifunga CBE ya Ethiopia kwa penalti 5-4 katika Uwanja wa Njeru, Uganda leo.

Kwa ubingwa huo JKT Queens itawakilisha Cecafa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Ivory Coast, Novemba mwaka huu.

Katika mchezo huo ambao ulioneshwa na Fufa tv ya mtandaoni ulishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 120 bila kufungana na ubingwa kuambuliwa na mikwaju ya penalti.

Mshindi wa tatu imechukuliwa na Buja Queens ambayo iliifunga Vihiga Queens ya Kenya kwa bao 1-0 nlililofungwa na Lydia Akoth dakika ya 41.

JKT Queens ambayo ilicheza fainali kwa mara ya kwanza ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Buja Queens ya Burundi kwa mabao 3-1 huku CBE ya Ethiopia ikiiondosha Vihiga Queens ya Kenya kwa mabao 2-1.

Tangu kuanzishwa kwa mashindano haya ni mwaka wa tatu na mabingwa ni Vihiga Queens, Simba Queens msimu uliopita na sasa JKT Queens.

Licha ya kuwa bingwa JKT Queens ilitoa mchezaji bora wa mashindano Stumai Abdallah na kipa bora Najiath Abbas.

No comments:

Post a Comment