Pages

Tuesday, May 8, 2018

WAANGOLA KUCHEZESHA YANGA VS RAYON CONFEDERATION

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeteua waamuzi wanne kutoka nchini Angola kuchezesha mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya makundi kati ya Yanga na Rayon unaotarajiwa kuchezwa Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao utaanza saa 1:00 usiku utachezeshwa na mwamuzi ni Helder Martins Rodrigues akisaidiwa na Ivanildo Meirelles De O Sanche na Wilson Valdmiro Ntyamba  na mezani atakuwepo Joao Amado Muanda, kamishna atakuwa Abebe Solomon Gibresilassie kutoka Ethiopia.
Awali mchezo huo ulikuwa uchezeshwe na waamuzi kutoka Kenya lakini wambedalishwa kutokana na timu ya Gor Mahia kuwa kundi moja na Yanga na Rayon pamoja na USMA Algier.
Yanga itakutana na Rayon ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa USMA Algier wakati Rayon walitoka sare na Gor Mahia.
Wakati huo huo TFF imeitaka Yanga pamoja na AFC ya Arusha na Coastal Union ya Tanga kufanya uchaguzi kujaza nafasi za viongozi wake waliojiuzulu
Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Manji aliingia Yanga mwaka 2006 kama mdhamini kupitia kampuni yake ya Lotto Kitita, lakini baadaye akawa mfadhili Mkuu wa klabu kabla ya kuwa Mwenyekiti.

No comments:

Post a Comment