Pages

Friday, May 11, 2018

MALIMA WA MBEYA CITY AFUNGIWA MECHI TATU, YONDANI NA CIAOBA WAIKACHA KAMATI YA NIDHAMU



KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mipira wa Miguu (TFF) imemfungia mechi tatu na kumpiga faini ya Sh. 500,000 beki wa Mbeya City, Ramadhani Malima kwa kitendo cha kuingia uwanjani kushangilia bao baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City April 22 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Akizungumza na wandishi wa habari leo, Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema kamati hiyo ilikutana Mei 9 na kusikiliza mashauri manne tu huku kocha wa Azam Ciaoba na beki wa Yanga Kelvin Yondani wakishindwa kufika katika kamati hiyo bila taarifa
 “Ramadhani Malima alitolewa kwa kadi nyekundu lakini baada ya timu yake kusawazisha bao mchezaji huyo alionekana uwanjani akishangilia na wachezaji wengine,”
“Kutokana na kosa hilo Malima amefungiwa mechi tatu ambayo mechi moja ameshaitumikia hivyo zimebaki mechi mbili na faini ya kiasi cha Sh. 500,000 "alisema Ndimbo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Shomari Lawi wa Kigoma akisaidiwa na Omar Juma wa Dodoma na Godfrey Kihwili wa Arusha, Yanga ilitangulia kufunga bao kipindi chake cha kwanza lililofungwa na  Raphael Daudi kabla ya Mbeya City kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Iddi Suleiman Nado.
Malima alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kumfuatia kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Yussuf Mhilu, lakini akarejea uwanjani kushangilia bao la kusawazisha la timu yake katika dakika za mwishoni.
Pia kamati hiyo imewafungia kucheza mechi tatu na faini ya Sh. 300,000 kila mmoja kutokana na kwa kitendo cha kutaka kumpiga mwamuzi katika mchezo wa Ligi daraja la pili dhidi ya Namungo FC
Naye Katibu wa Mlandizi Queens, Rukia Michael amefungiwa miezi miwili na kutozwa faini ya Sh. 200,000 kwa kosa la kutaka kumpiga mwamuzi  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya timu yake na Kigoma Sisters uliochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani.
Mashauri mengine kadhaa hayakusikilizwa baada ya kutofika kwa washtakiwa wa mashauri hayo na kamati imeomba wapewe wito wa mwisho ambao kama hawatafika kamati itasikiliza mashauri yao katika upande mmoja na kuyatolea maamuzi.

Ambao hawakufika na hawakutoa taarifa ni George Rast na Shaibu Salim(AFC-Wachezaji),Aristica Cioaba(Azam FC-Kocha),Issa Ngwasho(JKT Mlale-Meneja),Hosea John,Rashid Ally,Hamis Athuman,Casmir Focus(JKT Msange-Wachezaji),Joseph Mkota(JKT Oljoro-Mchezaji),Katregea Kalegea(Mashujaa FC-Mchezaji),Cuthbet Japhet(Toto Africans-Afisa habari),Kelvin Yondan(Young Africans-Mchezaji) wakati Meneja wa Singida United Ibrahim Mohamed yeye alitoa taarifa ya kufiwa na baba yake mzazi.


No comments:

Post a Comment