Pages

Friday, February 9, 2018

MWAKYEMBE ATEUA KAMATI YA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametua kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini Tanzania.
Akizungumza jana, Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja alisema kamati hiyo ina wajumbe 12 na itakuwa ikisaidia Baraza la Michezo la Taifa kuratibu shughuli za kila siku za ngumi za kulipwa nchini Tanzania
“Januari 3, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe aliteua wajumbe kumi na mbili kuunda kamati ambayo ingetengeneza Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa nchini Tanzania na ilikabidhi rasimu Februari 3,” alisema Kiganja.
“Baada kuipokea Rasimu hiyo aliipongeza na kuishukuru kamati hiyo  kwa kazi nzuri iliyofanya kwa umahiri na kujitoa kwa muda wao na kuahidi kuwa atateua kamati nyingine ambayo ndio hii ninaitangaza leo,” aliongeza Kiganja
Kamati hiyo Mwenyekiti Emmanuel Saleh, Makamu Mwenyekiti ni Joe Anea na Katibu ni Yahya Poli
Wajumbe ni Habib Kinyogoli, Rashid Matumla, Anthony Ruta, Shomari Kimbau, Dk.Killaga Killaga, Karama Nyilawila, Fike Wilson, Jaffar Ndame na Ali Bakari                                                                 
Kigamnja alisema kamati hiyo itapokea maoni kwa maandishi kutoka kwa wadau wa ngumi katika kipindi cha mwezi mmoja kupitia tovuti ya Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz na tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz

Pia itaratibu mkutano wa kujadili rasimu katika kipindi cha miezi miwili ili kuwapa wadau waliokosa nafasi kwa njia ya maandishi kutoa maoni yao na kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment