Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 18, 2018

SIMBA YANOGA, YAISAMBARATISHA SINGIDA UNITED KWA MABAO 4-0




SIMBA leo imejikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba ilianza kuandika bao katika dakika ya tatu ya mchezo baada ya Shizza Kichuya kufunga baada ya kutuliza mpira na kuujaza wavuni kwa juu.
Dakika nne baadae, Nicolas Gyan nusura afunge, lakini akiwa katika nafasi nzuri,alipiga mpira nje.
Asante Kwasi akiichezea Simba kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu tangu ajiunge nayo katika dirisha dogo la usajili akitokea Lipuli ya Iringa, alifunga katika dakika ya 24.
Wachezaji wa Singida walifikiri mfungaji atakuwa ameotea na kusita kumzuia na kupatikana kwa bao hilo.
Dakika ya 76, Emmanuel Okwi aliyeingia kipindi cha pili, aliifungia Simba bao la tatu na kuifanya timu hiyo kuzidi kuwa na uhakika wa kutoka na pointi zote tatu.
 Okwi ambaye alirejea juzi kutoka kwao Uganda, ambako alikaa zaidi ya muda alioruhusiwa, alifunga bao la nne baada ya kupata pasi kutoka kwa Ndemla baada ya kumkwepa kipa.
Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 29 baada ya michezo 13 na kuiacha Azam FC ya pili na pointi zake 27 huku Yanga ikibaki katika nafasi ya tano kwa pointi zake 22.
Azam  ambayo imekalia kwa muda kiti cha uongozi wa ligi baada ya kutoka sare ya 1-1 na Majimaji ya Songea katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji, huku Yanga jana ikilazimishwa suluhu na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Ushindi huo ulishuhudiwa na kocha mpya wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre aliyekuwa jukwaani wakati timu hiyo ikitoa kipigo hicho.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, klabu hiyo wakati wowote itaingia mkataba na kocha huyo aliyeipatia Cameroon ubingwa wa Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2000.
Vikosi vilikuwa, Simba: Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murdhid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/Mohamed Ibrahim, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin/Emmanuel Okwi.
Singida: Peter Manyika, Micahel Rusheshagonga, Shafik Batambuzi, Kenned Wilson, Maliki Antiri, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafwadza Kutinyu/Yusuph Kagoma, Lubinda Mundia/Kenny Ally, Kambale Salita na Kiggi Makasi/Elinywesia Sumbi.

No comments:

Post a Comment