Kocha mpya wa Simba, Pierre Lechantre na kocha wa viungo Mohammed Aymen Hbibi wakishuhudia timu hiyo Uwanja wa Taifa leo |
UONGOZI wa
Simba SC umeamua kuachana na kocha Hubert Velud na kumchukua Mfaransa mwenzake,
Pierre Lechantre.
Taarifa ya
klabu ya Simba leo kwa vyombo vya Habari imesema kwamba, kocha huyo mzoefu
ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha Mrundi, Masoud Djuma ambaye
amekuwa akiiongoza timu tangu Desemba mwaka jana alipoondolewa Mcameroon,
Joseph Omog.
Taarifa hiyo
imesema Lichantre amekuja na msaidizi mmoja, kocha wa viungo, Mmorocco Mohammed
Aymen Hbibi na jana aliishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Pierre
Lechantre aliyezaliwa Aprili 2, mwaka 1950 mjini Lille, Nord, Ufaransa ni kocha
aliyeipa Cameroon ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2000 na
kabla ya kuanza kufundisha alikuwa mchezaji pia.
Aprili 27
mwaka 2012, Lechantre alitambulishwa kuwa kocha mkuu wa Senegal, lakini
akashindwa kufikia makubaliano ya mwisho na Shirikisho la Soka la nchi hiyo.
Akiwa
mchezaji katika nafasi ya ushambuliaji, Lechantre amechezea klabu za Paris FC
(1986–1989),
Red Star 93 (1983–1986), Stade de Reims (1981–1983), Olympique de Marseille (1980–81)
na RC Lens (1979–80).
Zingine ni Stade Lavallois (1976–1979), AS Monaco
(1975–76),
FC Sochaux (1970–1975) na Lille OSC (1964–1970).
Na akiwa
kocha amefundisha timu za taifa za Kongo (2016), Cameroon (1999-2001), klabu za
Al-Ittihad Tripoli ya Libya kuanzia 2014 hadi 2015 na Al Arabi ya Qatar kuanzia
Machi hadi Septemba 2013.
Zingine
alizowahi kuzifundisha ni pamoja na CS Sfaxien ya Tunisia kuanzia Juni hadi
Desemba 2010, Club Africain ya Tunisia kuanzia Juni 10 mwaka 2009 hadi Aprili
2010 na Al Rayyan ya Qatar.
Amefundisha
pia timu ya taifa ya Mali kuanzia Machi hadi Oktoba 2005, Al-Siliya Sports Club
ya Qatar kuanzia Novemba 2003, Al-Ahli ya Jeddah kuanzia Agosti hadi Oktoba
mwaka 2003, Qatar kuanzia Juni 2002, Le Perreux (1992–1995)
na Paris FC (1987–1992).
Amewahi pia
kuwa Mshauri wa Ufundi wa Val de Marne kuanzia Julai 7 mwaka 1995 hadi Januari
1999.
Na ujio wa
kocha huyu unazima mpango wa kocha wa zamani wa TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Etoile du Sahel ya Tunisia, Mfaransa, Hubert
Velud kujiunga na Simba.
Habari za
ndani zinasema kwamba, Velud ni pendekezo la Mjumbe Mteule wa Kamati ya
Utendaji ya Simba, Mohammed Nassor ‘Mohaamed Kigoma’
ambaye alipambana mno klabu imchukue mwalimu huyo, lakini akakutana na upinzani
mkali kutoka kwa Kaimu Rais, Salim Abdallah.
No comments:
Post a Comment