KAMATI ya saa 72 imetupa malalamiko ya Dodoma
FC dhidi ya JKT Oljoro katika mechi iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja
wa Ushirika mjini Moshi.
Akizungumza leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi
ya Ligi (TPBL) Boniface Wambura alisema malalamiko hayo yalikuwa na sehemu
mbili; moja ni uhalali wa mchezaji wa JKT Oljoro, Haki Rubea kuwa hakuwa na
leseni, na mbili ni kudai kuwa Mwamuzi na Mwamuzi Msaidizi namba moja walikataa
bao lao halali.
“Baada ya kupitia malalamiko hayo, Kamati
imebaini kuwa Haki Rubea ni mchezaji wa JKT Oljoro mwenye leseni namba
961111011 iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hivyo ni
mchezaji halali,” alisema Wambura
Pia Wambura alisema kamati haina mamlaka ya
kukubali bao ambalo limekataliwa na mwamuzi uwanjani, hivyo kamati imetupa
malalamiko ya Dodoma FC kwa hoja zote mbili.
Aidha Wambura alisema kamati imejiridhisha
kuwa Kamishna wa mechi hiyo Paul Opiyo na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina
walifanya makosa kumruhusu mchezaji huyo kucheza bila kuonyesha leseni yake.
Alisema kamati imeteua wajumbe watatu kupitia
mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha
uchezeshaji cha mwamuzi msaidizi, Emmanuel Muga na mwamuzi wa akiba, Gilbyrth
Mrina na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua zaidi na tayari
wameondolewa kwenye ratiba kutokana na kupata maksi chache.
Wakati huo huo timu mbalimbali za daraja la
kwanza, viongozi na wachezaji wametozwa faini kutokana na makosa mbalimbali.
Wachezaji wa Friends Rangers Almasi Mkinda na Mtoro
Hamisi, wamefungiwa mechi tatu na faini y ash. 300,000 kila mmoja na Prosper
Mushi wa African Lyon wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000
African Lyon imepigwa faini ya sh. 600,000
baada ya kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi moja na kugoma kuingia
vyumbani, JKT Tanzania imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake
kuingia eneo la kuchezea kushangilia ushindi
Nayo Polisi Tanzania imepigwa faini ya jumla
ya sh. 1,000,000 kutokana na gari la washabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani na
kuzunguka uwanja wakati timu zikifanya mazoezi na wakati wa mapumziko na baada
ya mchezo kumalizika washabiki wa timu hiyo waliwafuata waamuzi na kutaka kuwapiga.
Alliance Schools imepigwa faini ya sh. 500,000
kutokana na timu yake kutoingia vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari
13, 2018 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
No comments:
Post a Comment