Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 27, 2018

NYOSO APELEKWA KAMATI YA MAADILI

KAMATI ya uendeshaji wa ligi imempeleka beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso katika kamati ya nidhamu pamoja na kocha wa Mbeya Kwanza Maka Mwalwisi
Nyoso anatuhumiwa kumpiga shabiki baada ya mchezo dhidi ya Simba na Kagera Sugar na kuzimia na kulazimika kulazwa hospitali kwa siku kadhaa na yeye kushikiliwa na polisi na Maka anatuhumiwa kuwashambulia viongozi wa TFF akidai wanaandaa timu za kupanda Ligi Kuu, ndiyo maana waamuzi wananyonga haki yao ya kupata ushindi.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPBL) Boniface Wambura alisema kuwa kamishna wa mchezo huo ameripoti kuwa Nyoso alimpiga shabiki huyo hivyo kamati ya saa 72 imempleleka kamati ya nidhamu ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa zaidi za kinidhamu.
“Kamati  ya saa 72 imepeleka swala la beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso katika kamati ya nidhamu kwa ajili ya hatua zaidi na kocha Maka anatakiwa kuthibitisha kauli yake aliyotoa baada ya kumalizika mchezo uliochezwa Januari 13, 2018 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,” alisema Wambura.
Wengine waliopelekwa katika kamati hiyo ni daktari wa viungo wa Rhino Rangers, Ahamad Mgongo na kipa Mohamed Ibrahim Salumu wa timu hiyo na wachezaji Mohamed Suleiman Ussi, Khalid Mahmud Konobile, Abubakar Ramadhan na Victor William Alimwene wa Transit Camp na Gideon Joram Richard wa The Mighty Elephant.
Wakati kamati ya saa 72 ikimpeleka Nyoso katika kamati ya nidhamu uongozi wa Kagera umekaririwa ukisema hautamchukuliwa hatua mchezaji huyo.
Beki huyo mwaka 2015 aliwahi kufanya kitendo cha udhalilishaji kwa mshambuliaji wa Simba John Bocco wakati akiwa Azam FC, na kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilimfungia miaka miwili na faini ya Sh 2,000,000 alipokuwa Mbeya City.

Kulingana na kanuni ya 11 (37) inayozungumzia udhibiti wa adhabu kwa wachezaji, kipengele cha tano kinasema mchezaji atakayefanya kati ya yafuatayo atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini sh. 500000.

No comments:

Post a Comment