Mgambo, Mshikamano zenye pointi sawa 15 na
Kiluvya yenye pointi 17 hata zikipata matokeo mazuri hazishuki wala hazipandi.
Mshikamano itachuana dhidi ya Kiluvya United. Ingawa Kiluvya itakuwa ina nafasi
kama Lyon na Friends Rangers zitafungwa michezo yote ya mwisho.
Pages
▼
Friday, January 26, 2018
LEO NDIO LEO LIGI DARAJA LA KWANZA KUNDI A NA KUNDI C
PRESHA
inapanda na kushuka kuelekea lala salama ya Ligi Daraja la Kwanza kwa timu za
Friends Rangers, African Lyon, zinazotafuta nafasi moja kupanda Ligi Kuu, huku
Ashanti na Mvuvumwa zikipigania kutoshuka daraja Kundi A.
Tayari JKT Tanzania imekata tiketi ya kucheza
Ligi Kuu msimu ujao kutoka katika Kundi A baada ya kucheza michezo 12,
kufikisha pointi 31, ambazo haziwezi kufikiwa na yeyote katika michezo miwili
kila mmoja aliyobakiza.
Mchezo wa leo, JKT Tanzania dhidi Friends
Rangers kwenye Uwanja wa Mbweni, utatoa taswira baada ya matokeo.
Lakini presha itakuwa kubwa hasa kwa Rangers
yenye pointi 22 kutafuta matokeo mazuri ingawa JKT imekuwa ni timu ngumu
kufungika hasa kwenye uwanja wake.
Pia, kazi ni kubwa zaidi kati ya Ashanti United
dhidi ya African Lyon kwa kuwa zote zitapigana kupata matokeo mazuri, Lyon
ikitafuta nafasi ya kupanda Ligi Kuu na Ashanti ikipigania kutoshuka daraja.
Lyon ina pointi 21 tofauti ndogo na Rangers na
zote kila mmoja anamuombea mwenzake mabaya, mmoja akishinda michezo hiyo na ile
ya mwisho ni faida kwa mwingine, zikitoka sare au kupoteza kazi itakuwa nzito
na pengine zikija kulingana pointi tofauti ya mabao itaamua baada ya mchezo wa
mwisho.
Ashanti United ina pointi tisa na Mvuvumwa
pointi nne, hivyo kushuka kwao kutategemea na nani amemzidi mwenzake baada ya
michezo miwili ya mwisho.
Mvuvumwa ikifungwa ugenini kwenye uwanja wa
Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo Shooting yenye pointi 15, itajiweka kwenye
hatari zaidi ya kushuka daraja. Hata ikishinda pia, haisaidii labda imuombee
Ashanti ipoteze michezo yote na yeye ashinde
ndiyo atanusurika.
Katika mechi za Kundi C, ambazo zitachezwa pia
leo, kazi ipo kubwa kwa Biashara, Alliance na Dodoma FC, ambapo timu mbili za kwanza ndizo zitapanda
daraja.
Kinara wa kundi ni Biashara yenye pointi 24,
Alliance yenye pointi 22 sawa na Dodoma
yenye pointi 22, huku Toto Africans, Pamba, Transit Camp na Oljoro zikipigania
kutoshuka daraja.
Biashara itacheza leo dhidi ya Oljoro mchezo
ambao ni mgumu ikiwa kwenye uwanja wa ugenini Moshi kwa kuwa kila mmoja atakuwa
ana kazi ya kutafuta pointi za kumwezesha kufikia malengo yake.
Alliance ina nafasi ya kufanya vizuri kama
itatumia vyema uwanja wake wa nyumbani kupata matokeo mazuri ila bado hautakuwa
rahisi kwa sababu Pamba inataka matokeo kupigania nafasi ya kutoshuka daraja.
Dodoma pia, ina nafasi ya kufanya vizuri kama
itatumia vyema uwanja wake wa nyumbani kupata matokeo dhidi ya Trans Camp
lakini vile vile, Camp inahitaji matokeo kujihakikishia nafasi ya kutoshuka
daraja, na Toto Africans isipojitahidi dhidi ya Rhino Rangers iko hatarini
zaidi kushuka kwani ndiyo inayoshikilia mkia.
No comments:
Post a Comment