Pages

Wednesday, October 11, 2017

TANZANITE QUEENS KUPAMBANA NA SIMBA QUEENS KUWANIA KUPANDA LIGI KUU YA WANAWAKE



TIMU ya Tanzanite 2014 ya Arusha inaongoza kundi la Dar es Salaam kwa pointi sita baada ya jana kuifunga Kisarawe Queens mabao 15-0 katika mchezo wa ligi ndogo ya wanawake uliochezwa katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. 

Katika mchezo mabao ambao ulikuwa wa upande mmoja Tanzanite 2014 ilikuwenda mapumziko ikiwa na mabao 6-0 na kipindi cha pili cha pili ikafunga mabao 9-0

Katika mchezo huo mshambuliaji Rukia Hussein alifunga hat trick ya mabao matano, Eva Emanuel na Tatu Idd akafunga hat trick ya mabao matatu, Agnes Sawe na Anitha Anthony wakafunga mabao mawili kila mmoja.

Kwa matokeo hayo Tanzanite 2014 inaongoza ikiwa na pointi sita sawa na Simba Queens lakini ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufugwa.


Kesho Simba Queens itamenyana na Tanzanite 2014 na mshindi wa mchezo huo ndio atapanda kucheza ligi kuu ya wanawake na mchezo mwingine utakuwa kati ya Moro Sisters dhidi ya Kisarawe Queens ambao haina pointi.
Katika kituo cha Dodoma Alliance Schools inaongoza ikiwa na pointi sita ikifuatiwa na Unyanyembe ya Tabora ambayo ina pointi sita.

No comments:

Post a Comment