Pages

Wednesday, October 11, 2017

MESSI AIPELEKA ARGENTINA KOMBE LA DUNIA

Lioneil Messi alfajiri ya leo ameipeleka Argetina katika michuano ya kombe la dunia mwakani, hii inaifanya michuano hii kuwa na Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi lakini kuna wachezaji 11 wakubwa ambao wanakosa michuano hii.
Jan Oblak. Akiwa na miaka 24 tu tayari mlinda lango huyu anatajwa kama kati ya makipa bora kuwahi kutokea La Liga, pamoja na ubora wake lakini ameshuhudia Slovenia ikikosa michuano ya kombe la dunia.
Antonio Valencia. Mlinzi wa kulia wa Manchester United ambaye ni kati ya wachezaji tegemezi Ecuador, alfajiri ya leo wamekula bao 3 lakini hata kabla walikuwa tayari wameshakosa tiketi.
David Alaba. Upande wa kulia yupo Alaba ambaye anacheza katika kiwango cha juu sana akiwa na Bayern Munich lakini pamoja na uwezo wake ameshindwa kuisaidia Austria kwenda Urusi mwakani.
Virgil Van Dijk. Katika dirisha hili la mwisho la usajili jina lake limekuwa likitajwa sana kutokana na uwezo wake lakini yeye na Uholanzi hawajafanya jambo kubwa la kuwapa tiketi kwenda kombe la dunia.
Gary Medel. Hili linaweza kuwa jina kubwa kwa wengine lakini Medel anayeichezea Bestikas kwa sasa ni kati ya walinzi hodari sana katika bara la Ulaya hivi sasa,  lakini ameshindwa kuizuia Chile isitolewe.
Naby Keita. Mashabiki wa Liverpool wanamjua vyema huyu kiungo kutokana na walivyohangaika kumpata, lakini baada ya Guinea kukosa tiketi ya kombe la dunia ina maana Keita ataangalia michuano hiyo kideoni.
Artulo Vidal. Kiungo mwingine wa kati kutokea Bayern Munich, Vidal ana uwezo mkubwa sana uwanjani lakini ameiangusha Chile katika kufuzu kwenda kombe la dunia.
Gareth Bale. Nyota wa kiwango cha dunia anayekipiga Real Madrid, wakati CR7 anakwenda kombe la dunia itabidi Bale aangalie tu baada ya Wales kushindwa kufuzu.
Christia Pulisic. Huyu anaitwa Lioneil Messi wa Marekani, yupo katika kiwango kikubwa sana lakini pamoja na kufunga bao moja alfajiri lya leo alishuhudia Panama wakikata tiketi kwenda Urusi.
Alexis Sanchez mwanazoni alikuwa na matumaini kwenda kombe la dunia lakini kipigo cha bao 3 toka kwa Brazil kilikata ndoto na matumaini ya mshambuliaji huyu wa Brazil.
Pierre Aubemayang. Anaongoza katika ufungaji Bundesliga lakini ameshindwa kuiongoza Gabon kwenda kushiriki kombe la dunia, hadi sasa iko wazi kwamba Aubemayang hatakwenda Urusi kushiriki kombe la dunia

No comments:

Post a Comment