Pages

Tuesday, October 3, 2017

SPANEST BAND KUHAMASISHA UTALII NA KUPIGA VITA UJANGILI

Mratibu wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki akiwa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya Nyanda za Juu Kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la Parokia ya Kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
SPANEST Band wakitumbuiza wakati wa maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

SPANEST Band ya mkoani Iringa yaendelea kutoa elimu ya utalii na kupiga vita ujangili kwa watanzania kupitia nyimbo mbalimbali ambazo zimekuwa zikihamasisha wananchi kuujua utalii,kutunza vivutio vyote vya kitalii na kuacha kuuwa wanyama wanaoendelea kuliingizia taifa pato kupitia utalii.
 
Akizungumza na blog hii mratibu wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki alisema kuwa wameamua kuanzisha Band hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya utalii na kupiga vita ujangili kwa njia ya sanaa ili kuwafiki wananchi walio wengi.

“Unajua kuwa watu wengi wanapenda kusikiliza nyimbo na kuona maenyesho ya wasanii hivyo uwepo wa SPANEST Band umesaidia kutoa elimu ya utalii ndio maana unaona kwenye maonyesho mengi wakuwa wakitumbuiza na kupendwa na kila mtu anayekuwa katika eneo hilo” alisema Meing’ataki.

 Meing’ataki alisema kuwa nyimbo za SPANEST Band zinatoa elimu mahususi ya maswala ya utalii hivyo imekuwa kazi rahisi kuwafika vijana na watu wengine wa rika mbalimbali ambao wamekuwa wakihudhuria matamasha au maonyesho ya kitalii.

Aidha Meing’ataki alisema kuwa Band hiyo tayari imeshasajili na baraza la Sanaa na michezo (BASATA) hapa nchi ili kupata fursa ya kutumbuiza katika maonyesho yoyote hapa nchini na kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa watanzania na wasio watanzania.

“Usiposajili kazi yako utakuwa unajinyima haki yako ya msingi hivyo band hii ya SPANEST imesajili na BASATA wanaijua hivyo kuifanya kufanya hata kazi za serikali kwa kuwa waandaa nyimbo zao bila kukiuka sheria za nchi” alisema Meing’ataki

Meing’ataki aliwaomba wadau mbalimbali wa utalii na uhifadhi kuendelea kuiunga mkono SPANEST Band ili wapate nafasi ya kuendelea kutoa elimu kwa njia ya Sanaa ya uimbaji ambao kwa kiasi kikubwa kwa sasa vijana wengi wanaitumia.

“Mimi nawapongeza sana wasnii wote wa SPANEST Band kwa kazi wanaifanya kuelimisha jamii kwani wanatunga nyimbo zao vizuri na zinahamasisha wananchi kupembela vivutio vyao na kupiga vita ujangili wa wanayama ambao ndio vituo vikubwa kwenye mbuga zetu hapa nchini” alisema Meing’ataki

Naye katibu wa band hiyo Denis Nyali alisema waliamua kuanza kuandaa nyimbo za kuhamasisha utalii na kuacha kuuwa wanyama kutoka na kufanya utalii katika mbuga mbalimbali na kijionea vitu vingi ya kuvutia.

“Mimi ni mwandishi wa habari hapa mkoani Iringa tulikuwa tumeenda kutalii katika mbuga ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa tukapewa zoezi la kutafuta njia za kutoa elimu ya kupinga ujangili na kutoa elimu ya utalii na ndio ulikuwa mwanzo wa kuanzisha SPANET Band” alisema Nyali

Nyali alimpongeza mratibu wa mradi wa SPANEST Godwell Ole Meing’ataki ambaye pia ni mwenyekiti wa Band hiyo kwa juhudi zake za kuanzisha na kuendeleza kwa kuwaongezea majukumu ya kutumbuiza kwenye matasha mbalimbali ya utalii na kuzifanya nyimbo zake kuwa maarufu.

“Unajua sisi ni wasanii tu hivyo bila kuwa na mtu anayetusaidia hatuwezi kufika popote pale ndio maana kushikwa mkono na mratibu wa mradi wa SPANEST Ole Meng’ataki kumetusaidia kuendelea kutunga nyimbo na kufanya video za nyimbo hizo ambazo zimekuwa na mvuto kwa jamii” alisema Nyali

Nyali alisema kuwa lengo la Band hiyo ni kuendelea kutoa elimu ya kitalii kwa kutumia nyimbo ambazo wanazoziimba kwa njia tofauti tofauti kufikisha ujumbe halisi kwa wanachi waupende utalii na kupiga vita ujangili ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya utalii.

“Tunawaomba wananchi wawe na subila hivi karibuni tutawaambia kuwa nyimbo hizi zitapatikana wapi kwa kuwa Band hii ipo chini ya mratibu wa mradi wa SPANEST hivyo tunasubili muungozo wa kutoka kwao kwa kuwa kazi yetu tumeshamaliza ya kurekodi na tunaendelea kutumbuiza katika maonyesho mbalimbali ambayo tunakuwa tunaalikwa” alisema Nyali

No comments:

Post a Comment