Pages

Sunday, October 8, 2017

SIMBA QUEENS YAICHAPA KISARAWE QUEENS MABAO 8-0 LIGI YA WANAWAKE




SIMBA Queens imeanza vema mashindano ya ligi ndogo ya wanawake baada ya kuifunga Kisarawe Queens mabao 8-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao ulichelewa kuanza kutokana na Kisarawe kuchelewa kufika uwanjani huku wakiwa pungufu, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 5-0.
Kipindi cha pili Simba ambao wanaonekana kujiandaa vema waliongeza mabao matatu yalifanya waondoke na karamu ya mabao katika mchezo huo wa ufunguzi
Akizungumza Katibu wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) Somoe Ng’itu alisema awali ligi hiyo ilikuwa ishirikishe timu 14 ambazo zimegawanywa katika makundi mawili.
“Timu 14 zilithibitisha kushuriki lakini hadi leo ligi inaanza timu nane pekee ndio ambazo zimefika katika kituo cha Dodoma nne na Dar es Salaam nne,” alisema Somoe.
Katika kituo cha Dar es Salaam timu zilizofika ni Simba Queens, Kisarawe Queens, Moro Sisters na Tanzanite 2014 na ambazo hazijafika ni Mbinga Queens, Kilimanjaro SC na Kwakaeza Women.

Kituo cha Dodoma timu zilizofika ni Allans, Alliance Queens, Songwe na Mapinduzi Queens wakati ambazo hazijafika ni Kasulu SA, Mbesco na Unyanyembe Queens.

No comments:

Post a Comment