Pages

Wednesday, October 4, 2017

JULITHA KABETE KUIWAKILISHA TANZANIA MISS WORD 2017 CHINA


Mrembo Julitha Kabete (Katikati) mara baada ya kushinda taji la miss Ilala mwaka jana.
******************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited ambayo inaandaa  mashindano ya urembo ya Miss Tanzania imemteua Julitha Kokumanya Kabete kuwaikilisha Tanzania katka mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika Sanya, nchini China mwezi ujao.
Afisa Habari wa Lino International Agency Limited, Hidan Ricco amesema kuwa tayari jina la mrembo huyo limekwishwa wasilishwa kwa waandaaji wa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika  Novemba 18, kwenye ukumbi wa Crown of Beauty Theatre.
Ricco amesema kuwa  mrembo huyo ambaye ni ambaye ni mshindi wa shindano la Miss Dar Centre,  Miss Ilala na mshindi wa tano wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka jana,  kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo.
Alisema kuwa uteuzi wa Mrembo Julitha Kabete umezingatia uzoefu wa mashindano ya urembo alionao, uwezo wake katika Tasnia ya urembo, uelewa wa vivutio vya utalii na raslimali tulizonazo hapa nchini, pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyonayo mrembo huyu tangu mwanzo anashiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania katika ngazi ya Kitongoji, Mkoa, Kanda hadi Fainali za Taifa kwa mwaka 2016.
“Julitha  pia alipata fursa ya kushiriki mashindano ya urembo ya Afrika 2016 (Miss Afrika 2016) yaliyofanyika nchini Nigeria na alituwakilisha vizuri tu, na hivyo kupata uzoefu wa kutosha, jambo ambalo pia litaongeza uwezo wake wa kutuwakilisha vema katika Mashindano ya urembo ya Dunia 2017,” alisema Ricco. 
Mashindano ya Miss Tanzania yanayoendelea katika sehemu mbalimbali ambapo fainali zake zitafanyika hapo baadaye.
Alisema kuwa mshindi wa mwaka huu atawakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia hapo mwakani 2018, hivyo kupata muda wa kutosha wa matayarisho.
“Hii sio mara ya kwanza kwa mrembo wa Taifa wa mwaka huu kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Dunia mwaka unaofuata, mwaka 2012 Miss Tanzania Brigitte Alfred aliwakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2014,” alisema Ricco.
Mrembo pia atakabidhiwa Bendera ya Taifa na Kiongozi wa Serikali ambaye tutamtambulisha hapo baadae
Kwa hisani ya Sufiani Mafoto blog.

No comments:

Post a Comment